Friday, October 17, 2014

Friday, October 17, 2014

MATUMIZI ya mafuta ya petroli na dizeli yamezidi kuongezeka nchini huku kampuni ya Camel Oil ikiongoza kampuni za kizalendo kwa kuagiza kiasi kikubwa mwaka huu ikitokea nafasi ya saba mwaka jana.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati (Ewura), ya ‘Petroleum Industry Performance’ kuanzia Julai 2013 hadi Juni mwaka huu, jumla ya lita 2,938,896,540 za mafuta ya aina mbalimbali ziliagizwa na kutumika.
Kiasi hicho ambacho ni wastani wa lita bilioni 3, ziliagizwa na jumla ya kampuni 17 za mafuta na kuuzwa hapa nchini na kumekuwa na ongezeko la asilimia 10 ya mahitaji ya mafuta nchini.
Takwimu za Ewura zinaonyesha kuwa kwa mwaka ulioanzia Julai 2012 hadi Juni 2013, jumla ya mafuta yaliyoagizwa na kuuzwa katika maeneo mbalimbali nchini yalifikia wastani wa lita 2,672,389,280.
Takwimu hizo zinaonyesha kuwa kwa mwaka ulioishia Juni mwaka huu, kumekuwa na ongezeko la lita milioni tatu kulinganisha na mafuta yaliyoagizwa mwaka 2012/2013.
Taarifa hiyo ya Ewura inayoishia Juni mwaka huu, ilitaja kampuni zilizoongoza kwa uagizaji mafuta kwa wingi kuwa ni Puma ya Uingereza ambayo iliagiza lita 342,941,136 na Oryx ya Uswisi iliyoagiza lita 302,528,692.
Kampuni ya Camel Oil imeshika nafasi ya tatu ikitoka nafasi ya saba mwaka 2013 kwa kufanikiwa kuagiza lita 241,383,903 na kampuni ya Total ikiwa imeagiza lita 217,927,292.

CHANZO: Tanzania Daima

0 comments: