Wahudumu wa afya wakiwa kwenye kituo cha matibabu ya Ebola cha Madaktari wasio na Mipaka (MSF), kilicho ndani ya uwanja wa Samuel K. Doe jijini Monrovia,Liberia oktoba 15,2014.

MONROVIA, Alhamisi
Waziri mmoja nchini Liberia amesema kuwa ameamua kujitenga kwa hiari siku ya alhamisi baada ya dereva wake kufariki kwa ugonjwa wa Ebola ambao umeishambulia Afrika Magharibi.
Liberia imeathiriwa sana na janga hilo na imeripotiwa kuwa ugonjwa huo tayari umeshaua watu 2,458 kati ya wagonjwa 4,249 ambao kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya duniani(WHO), ni nusu ya kesi zote zilizowahi ripotiwa duniani.
Waziri wa uchukuzi Angela Cassell-Bush alisema ameamua kujitenga baada ya dereva wake kuugua kwa ugonjwa huo.
“Sikuwa na mgusano wa moja kwa moja nae bali ninafanya hivi kwa tahadhari” alieleza kwenye tarifa,akiongeza kuwa ataacha majukumu yake kwa siku 21 kufuatana na taratibu zinazokubalika za kiitifaki.
Haikufahamika mara moja ni lini dereva wake alifariki.
Viongozi wa dunia wameonya maambukizi ya Ebola yanaongezeka kwa kasi na kupelekea kuwa  tisho kubwa la kiafya ulimwenguni kwa miaka kadhaa.
Hadi kufika Jumapili watu 4,493 wameshafariki kati ya wagonjwa 8,997 tangu mlipuko wa Ebola ambao umezikumba nchi saba,kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni za WHO.
Rais waMarekani Barack Obama, jana alitoa mwito kwa dunia nzima kuchukua hatua zaidi,huku akisisitiza kuwa nchi yake itawajibika zaidi katika mwitikio wake, baada wa mhudumu wa pili wa afya kugundulika kuwa na ugonjwa huo huko Texas.

HOFU YAONGEZEKA ULIMWENGUNI
Hivi sasa ukweli kwamba mgonjwa wa hivi karibuni huko Dallas,ambaye ni mhudumu wa afya,alitumia usafiri wa anga ndani ya nchi kabla ya kutengwa siku hiyo,umeongeza hofu juu ya usafiri wa anga.
Maambukizi ya pili kwa mhudumu wa afya aliyemuuguza mgonjwa wa kwanza wa Ebola nchini Marekani yametilia shaka utayari wa nchi hiyo kupambana na ugonjwa huo unaoua.
Rais Obama alisema mwezi uliopita kuwa Marekani ilikuwa tayari kwa "tukio lisilowezekana" kwamba virusi vya Ebola vinavyoiangamiza Afrika Magharibi vinaweza kuingia nchini Marekani, na kwamba kila dharura itadhibitiwa kwa haraka.
Lakini wakati raia wa Liberia aliyekuwa na homa,maumivu ya mwili na kumbukumbu ya kutembelea nchi ambayo imeshambuliwa na maradhi hayo alipopelekwa kwa mara ya kwanza hospitalini Dallas tarehe 25/09/2014, alirudishwa nyumbani baada ya masaa manne.
Uamuzi huo unawaweka wagonjwa aliokuwa nao kwenye chumba cha matibabu ya dharura,wahudumu wa hospitali na familia yake kwa ujumla kwenye hatari ya kumbukizwa Ebola.
Baadae alirudishwa hospitalini hapo kwa gari la wagonjwa 28/9/2014,akiwa anatapika na kuharisha ambapo tayari alikuwa anaweza kuambukiza. Wengi wa wahudumu  wa afya wanaweza kuwa wameambukizwa kutokana na kutojikinga kwa usahihi.

CHANZO: AFP