Serikali inatarajia kuanzisha usafiri wa treni
kuanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere (JNIA) hadi katikati
ya Jiji la Dar es Salaam, ili kupunguza adha kwa abiria wanaosafiri kwa
ndege, ikiwa ni mkakati wa awali wa kuboresha na kuimarisha usafiri wa
abiria kwa wakazi wa Jiji hilo.
Maandalizi ya usafiri huo wa kilomita 13 unatarajia kukamilika Disemba mwaka huu na kubeba abiria 800 hadi 1,000.
Hayo yalibainishwa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk.
Shaaban Mwinjaka, na kuwa na kusema usafiri huo katika awamu nyingine
utakuwa ni kuanzia mjini kuelekea Gongo la Mboto, Bagamoyo, Kibaha na
Mkuranga.
Alisema kuwa wawekezaji ambao wamekwishafanya mazungumzo na serikali
katika miradi mbalimbali katika maeneo ya bandari za Dar es Salaam
pamoja na Mtwara ili kusaidia usafirishaji kutokana na kuwapo kwa
uchimbaji wa gesi mkoani humo.
Maeneo mengine ni viwanja vya ndege vya kimataifa nchini, usafiri wa
reli, soko la hisa pamoja na kuboresha kituo cha ukaguzi wa magari
katika Taasisi ya Taifa ya Usafirishaji (NIT).
“Soko la hisa linakua kwa kasi nchini, wawekezaji hawa 12 wametoka
nchini Marekani watakuwa katika miradi tofauti, na hii baada ya
mazungumzo kati yetu na Marekani, kwamba tunahitaji wawekezaji katika
maeneo tofauti na tulitoa kipaumbele katika kukabiliana na tatizo la
ajali za barabarani tutaboresha kituo cha ukaguzi NIT kwa kununua vifaa,
” alisema Mwinjaka.
Alisema katika kuboresha ukaguzi wa magari kupitia NIT ili kukabiliana
na ajali za barabarani, vinahitajika vifaa vya dola za kimarekani
milioni 50 sawa na Sh. bilioni 85, pia vitafunguliwa vituo vya ukaguzi
huo nchi nzima.
Pia alisema kuwa viwanja vya ndege vinavyopokea wageni wengi nchini kwa
siku, vinahitaji kuwa na sehemu ya malazi na kupumzikia wageni na kusema
ujenzi wa JNIA utakapokamilika utakuwa na huduma hiyo.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment