Katibu
Mkuu wa Chama cha ACT Tanzania, Samson Mwigamba akizungumza katika
mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana (hawapo pichani),
kuhusu maazimio ya mkutano wa tatu wa Kamati Kuu ya Chama cha ACT
Tanzania uliofanyika Jumamosi Oktoba 2014 katika Hoteli ya Vina jijini
Dar es Salaam.
|
Katibu
Mkuu wa Chama cha ACT Tanzania, Samson Mwigamba (katikati), akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana (hawapo
pichani), kuhusu maazimio ya mkutano wa tatu wa Kamati Kuu ya Chama cha
ACT Tanzania uliofanyika Oktoba,5, 2014. Kulia ni Katibu wa Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho, Mohammed Massaga na Katibu wa Ngome ya Vijana wa chama hicho, Philip Mallaki.
Wapiga picha wa vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Dotto Mwaibale
Katibu
Mkuu wa Chama cha ACT Tanzania, Samson Mwigamba amesema milango ipo
wazi kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto kujiunga na chama hicho
iwapo atapenda kufanya hivyo.
Mwigamba ameyasema hayo Dar es Salaam leo asubuhi wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati akitoa maazimio
ya mkutano wa tatu wa Kamati Kuu ya Chama cha ATC Tanzania uliofanyika
Jumamosi Oktoba 2014 katika Hoteli ya Vina jijini Dar es Salaam.
Alisema
Zitto anakaribishwa kujiunga na chama hicho iwapo atapenda kufanya
hivyo na sisi yeye tu hata wananchi wengine watakaopenda kufanya hivyo
kwani chama hicho licha ya kuwa na miezi michache tangu kuanzishwa kwake
kimepata wanachama zaidi 18,000.
“Chama
chetu kinamafanikio makubwa na kimekubali na watu wengi hivyo wanaotaka
kujiunga tunawakaribisha kwani tunawatu maarufu ambao tayari wamejiunga
” alisema Mwigamba.
Katika
hatua nyingine chama hicho kimesikitika na kushindikana kupatikana kwa
maridhiano baina ya makundi mbalimbali ya kisiasa nchini kuhusu mchakato
wa na maudhui ya Katiba Mpya.
“Kamati
kuu imesikitishwa zaidi na uamuzi wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali
yake wa kuteka na kuburuza mchakato wa katiba kwa kuegemea matakwa ya
sheria bila kujali uhalali mpana wa kisiasa na kijamii nchini.
Alisema
mchakato huo wa Bunge la Katiba umeitimishwa kwa mtindo ambao umeacha
mgawanyiko na mpasuko mkubwa wa kisiasa na kijamii nchini badala ya
kujenga umoja na mshikamano wa kitaifa, ambalo ndilo lengo la msingi la
mchakato wenyewe.
Mwigamba
alisema maazimio mengine yaliyofikiwa na kamati kuu ni kumtaka
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), atoe ripoti kuhusu
uchunguzi wa wizi wa fedha zinazodaiwa kuwa ni za umma uliofanyika
kupitia akaunti ya Escrow iliyotokana na mgogoro baina ya Tanesco na
IPTL.
Akizungumzia
kuhusu Bodi ya Mikopo kwa Vyuo vikuu, alisema wamesikitishwa na taarifa
kuwa zaidi ya wanafunzi 50 ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na vyuo
mbalimbali vya elimu ya juu nchini hawatapata mkopo.
Alisema
kamti hiyo haikubaliani na hali hiyo na inawahimiza wanafunzi,vijana na
wadau wa elimu nchini kuungana na chama cha ACT Tanzania katika
kuishinikiza Serikali kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapatiwa mikopo ili
waweze kuipata elimu ya juu ambayo inahitajika sana kwa mustakabali wa
nchi.
Mwigamba
alihitimisha taarifa yake kwa kusema uzinduzi rasmi wa chama hicho kuwa
utafanyika Desemba mwaka huu jijini Dar es Salaam katika eneo
litakalopangwa.
0 comments:
Post a Comment