MKANDARASI
Mkuu wa ujenzi wa Barabara ya Mabasi yaendayo Haraka (BRT), Strabag
International, ametangaza mabadiliko ya matumizi katika makutano ya
barabara za Morogoro na Kawawa.
Akitangaza mabadiliko hayo juzi jijini Dar es Salaam, Ofisa uhusiano
wa kampuni hiyo, Yahya Mkumba alisema, mabadiliko hayo yataanza kesho
Novemba 17 hadi 30 mwezi huu na yanatokana na matengenezo yatakayokuwa
yanafanyika eneo hilo.Mkumba alisema magari yatakayokuwa yanaelekea Ubungo kutokea Jangwani yatalazimika kutumia mchepuko uliopo kabla ya kituo cha Magomeni Mapipa kwa kuingia barabara ya mabasi yaendayo haraka.
Pia magari yatakayokuwa yanatokea Ilala Boma kuelekea Moroco, Ubungo na Jangwani, yatalazimika kutumia barabara moja ya upande wa kushoto.
“Wananchi watuvumilie katika kipindi hiki na tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaotokea,” alisema Mkumba.
Mradi wa BRT ambao umelenga kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam ambapo kilomita 20.9 za barabara kwa awamu ya kwanza zipo mbioni kukamilika kwa mujibu wa ratiba ya mkandarasi.
0 comments:
Post a Comment