Saturday, March 21, 2015

Saturday, March 21, 2015


Masheikh kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Bagamoyo, wamesema katika salamu zao kuwa wameona mtu pekee anayefaa kushika wadhifa huo ni yeye (Lowassa) hivyo wanamsihi atangaze nia na achukue fomu ya kugombea na wapo nyuma yake katika dua.

Lowassa amewaambia viongozi hao wa dini kuwa makundi mbalimbali ya jamii yamekuwa yakimuomba kugombea Urais lakini wao wamemfanya ashawishike sasa kufanya hivyo wakati ukifika.

"Ila nataka kuwaahidi, naheshimu sana maneno yenu na nayakubali kwamba siku ikifika kwa taratibu za chama nitachukua fomu,"alisema.

Lowassa amesema endapo Mungu atamjalia kushinda uchaguzi, atahakikisha anaendeleza pale Rais Jakaya Kikwete katika nyanja mbalimbali za Elimu, afya kilimo kwanza, na huduma nyingine muhimu kwa jamii. 

Lowassa amesema akifanikiwa nitaanza na elimu, na kufanya elimu kipaumbele chetu kwani elimu ndio msingi wa kila kitu.

 Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa (kushoto) akiwa amepokea fedha zilizo changwa na Masheikh kutoka Wilaya ya Bagamoyo. Walio mkabidhi fedha hizo ni Sheikh Yusuf Surul (kulia) na Ally Mtumwa. Mwingine ni Mbunge wa Urambo Magharibi, Prof. Juma Kapuya.

 MASHEKHE wakiwasili nyumbani hapo kwa ajili ya mazungumzo na Lowassa.

 Edward Lowassa akizungumza na Mashekhe hao mjini Dodoma.


 Masheikh hao kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Bagamoyo, Mlingotini, Kaole, Chalinze, Lugoba, Msata na kwingineko.

 
 Duaa ikisomwa na viongozi hao wa dini.

  Edward Lowassa akiwasindikiza viongozi hao.
 Lowassa akiagana na Sheikh Alli Mtumwa mmoja wa viongozi wa msafara huo.


 Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiagana na viongozi hao.

 Lowassa akimsikiliza mmoja wa Masheikh hao.

0 comments: