Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy
Akizungumza na kituo cha redio cha Clouds, Dar es Salaam jana, Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy alisema kuwa kila mtu anatakiwa kutambua kuwa anawajibika katika matumizi ya mawasiliano.
Mungy alisema TCRA kwa kushirikiana na serikali, wataiweka sheria hiyo kwenye mitandao na kwamba kila mmoja anapaswa kuisoma na kuielewa.
Pia alisema wanajiandaa kutoa elimu kuhusu sheria hiyo na jinsi watumiaji wa mitandao ya kijamii wanavyopaswa kujihadhari ili wasije kuwajibika.
0 comments:
Post a Comment