Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) limelaani vikali kitendo cha kushambuliwa na kupigwa kwa mwandishi wa habari wa magazeti ya Uhuru Publications Ltd Christopher Lissa na wanaodaiwa ni wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wiki iliyopita kwenye makao makuu ya chama hicho .
Akizungumzia tukio hilo leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Tanzania Bw. Absalom Kibanda (pichani kulia) amesema kitendo cha kupigwa kwa Lissa ni mwendelezo wa vitendo vyenye mwelekeo wa kuwazuia waandishi wa habari kutekeleza wajibu wao wa msingi wa kukusanya taarifa na kuuhabarisha umma .
Bwana Kibanda amewataka viongozi na wanasiasa kuwaacha wanahabari watekeleze wajibu wao bila kuwawekea vikwazo, na kwamba kuendelea kwa vitendo hivyo vya kuwapiga waandishi wa habari ni sawa na kujichukulia sheria mkononi jambo ambalo sio sahihi.
Hata hivyo,Bwana Kibanda amewataka waandishi wa habari kutokuonyesha hisia zao katika vyama vya siasa na hasa kupendelea upande mmoja wakati wanatekeleza wajibu wao wa kukusanya habari .
0 comments:
Post a Comment