Mwanamke mmoja, aliyetambulika kwa jina la Jiang Xulian,pamoja na mwanamme raia wa China wamekamatwa kwenye uwanja wa ndege wa Suvarnabhumi, Bangkok katika jitihada za kuondoka nchini Thailand, kufuatia wawili hao kutuhumiwa kuiba jiwe la almasi kwenye duka moja la kuuza madini. Inasemekana kuwa wawili hao waliingia kwenye duka la kuuza madini na kuomba kukagua almasi kabla ya kurudisha kipande kingine ambacho kilikuwa ni almasi bandia.
Almasi hiyo ina na thamani ya dola za kimarekani 278,000(sawa na shilingi za kitanzania milioni 556)
Awali katika mahojiano, watuhumiwa walikanusha kuhusika na tukio hilo kabla ya x ray kuonesha picha ya almasi tumboni kwa mwanamke huyo,ambapo baada ya ugunduzi huo mhusika akakiri.
Kwa mujibu wa polisi, kama wawili hao watapatikana na hatia basi watakabiliwa na kifungo cha miaka mitatu gerezani.
Kwa mujibu wa Kanali Mana, afisa wa polisi na mpelelezi mkuu wa kesi hiyo, mtuhumiwa alikubali kufanyiwa upasuaji huo jumapili baada ya kuambiwa kuwa anaweza kudhurika kiafya ikiwa jiwe hilo halitaondolewa.
Hata hivyo, mmiliki wa almasi hiyo aliweza kuitambua baada ya zoezi la upasuaji.
0 comments:
Post a Comment