Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange anasikitika kutangaza
kifo cha Meja Jenerali Aidan Isidore Mfuse (mstaafu) kilichotokea tarehe
29 Oktoba 2014 katika Hospitali ya Appolo nchini India alikokuwa
akipata matibabu.Mwili
wa marehemu Meja Jenerali Aidan Isidore Mfuse (mstaafu) unatarajia
kuwasili Tanzania tarehe 31 Oktoba 2014 saa 7:30 mchana na kuhifadhiwa
katika hospitali kuu ya Jeshi Lugalo. Heshima
za mwisho kwa Viongozi, Wanajeshi na Watumishi wa Umma zitatolewa
katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo tarehe 01 Novemba 2014, kuanzia saa
4.00 hadi saa 5.00 asubuhi na mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda
Njombe kwa mazishi, ambapo mazishi yanatarajiwa kufanyika tarehe 02
Novemba, 2014 saa 8.00 mchana.Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na MahusianoMakao Makuu ya Jeshi, Upanga
0 comments:
Post a Comment